Header Ads

DC Misungwi awatoa hofu wananchi “vyandarua haviondoi nguvu za kiume”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
BMG Habari
Mkuu wa Wilaya Misungwi mkoani Mwanza, Juma Sweda amewataka wananchi wilayani humo, kuhakikisha wanatumia vyandarua vilivyoboreshwa ili kujikinga na ugonjwa wa Malaria kwani vyandarua hivyo ni salama na havisababishi upungufu wa nguvu za kiume kama baadhi yao walivyokuwa wanadhani.

Sweda aliyasema hayo juzi katika Kata ya Mamaye kwenye zoezi la ugawanyi wa vyandarua vilivyowekewa dawa ya kuua mbu (vyandarua vilivyoboreshwa), zoezi ambalo limeratibiwa na shirika la PAMVECK Tanzania.

Wananchi katika Vijiji 72 vya Kata 17 wilayani Misungwi ambavyo kwenye utafiti wa awali vilionekana kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria, wamegawia vyandarua hivyo bure, lengo likiwa ni kuona namna vitakavyosaidia mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda akimkabidhi chandarua mmoja wa akina mama wilayani humo.
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Misungwi, Kisena Mabuba akimpongeza mmoja wa akina baba wilayani humo kabla ya kupokea chandarua chake.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda akizungumza wakati wa zoezi la ugawaji vyandarua vilivyoboreshwa wilayani humo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Misungwi, Kisena Mabuba akizungumza wakati wa zoezi la ugawaji vyandarua vilivyoboreshwa wilayani humo.
Viongozi mbalimbali wakishuhudia zoezi hilo.
Wananchi walifundishwa namna bora ya utumiaji vyandarua kabla ya kukabidhiwa.
Zoezi la ugwaji vyandarua vilivyoboreshwa wilayani Misungwi.
Zoezi la ugwaji vyandarua vilivyoboreshwa wilayani Misungwi.
Burudani na michezo mbalimbali ikiwemo ya kucheza na nyoka ilinogesha zoezi hilo.
Tazama BMG Online TV hapa chini
Taasisi ya APHFTA yasaidia mapambano dhidi ya Malaria
#PamojaDaimaBMG

No comments:

Powered by Blogger.