LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Biteko akutana na Mkurugenzi Mkuu NEMC

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Na Nuru Ikupa, Dodoma
Waziri wa Madini, Doto Biteko amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka Mafwenga, ofisini kwake jijini Dodoma.

Biteko ameshukuru Dkt. Mafwenga kwa kuonesha nia ya kuwasaidia wachimbaji wadogo kupata cheti cha mazingira baada ya kubainisha njia bora za kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata uelewa juu ya uhifadhi wa mazingira.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Januari jana, Dkt. Mafwenga alisema kutokana na mwamko mkubwa iliyonayo Serikali wa kuwasaidia wachimbaji wadogo kukua na kufanikiwa katika sekta ya uchimbaji mdogo wa madini, Nemc itajikita katika kuhakikisha inashirikiana na wizara katika kuhamasisha na kuelimisha wachimbaji wadogo juu ya umuhimu wa uhifadhi wa mazingira.

Aidha alibainisha kuwa, kutokana na vigezo vya awali ambavyo viliwafanya wachimbaji wadogo kutokupewa cheti cha mazingira zitaboreshwa na kuwawezesha kupata cheti hicho.

Alisema wachimbaji wadogo watapaswa kusajili miradi yao katika Ofisi za Kanda za Baraza la Hifadi la Mazingira  ambao watakagua miradi hiyo na baada ya kujiridhisha watawapatia vyeti hivyo.  
Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dr. Samuel Gwamaka Mafwenga (kulia) pamoja na Meneja wa Kanda ya Kati, Arnold Mapinduzi (kushoto) baada ya kumaliza mazungumzo mafupi ya namna ya kuwawezesha wachimbaji wadogo kuhifadhi mazingira.

No comments:

Powered by Blogger.