LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shirika la KIVULINI lajikita mkoani Kigoma kupambana na Ukatili wa Kijinsia

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Wasichana na Wanawake KIVULINI la Jijini Mwanza, Yassin Ally (kushoto), akitoa ufafanuzi wa shughuli zinazofanywa na shirika hilo katika Wilaya za Kibondo, Kakonko na Kasulu mkoani Kigoma baada ya Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mama Elizabeth Jacobsen (hayuko pichani) kufanya ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na Serikali ya Norway mkoani Kigoma, Januari 24, 2018.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Wasichana na Wanawake KIVULINI la Jijini Mwanza, Yassin Ally (kushoto), akiteta jambo na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mama Elizabeth Jacobsen (katikati) aliyefanya ziara mkoani Kigoma kukagua miradi inayofadhiliwa na Serikali ya Norway mkoani humo.
Shirika la KIVULINI linatekeleza mradi wa kuhamasisha jamii kupinga hadharani vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wasichana na wanawake katika Kata 10 za wilaya za Kibondo, Kakonko na Kasulu mkoani Kigoma.
Mwanaharakati wa kujitolea wilayani Kibondo, Rehema Mikidadi akieleza mafanikio yaliyopatikana kutokana na mafunzo yanayotolewa na shirika la KIVULINI katika kupambana na ukatili wa kijinsia mkoani Kigoma ikiwemo wanaume kutelekeza familia.
Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mama Elizabeth Jacobsen (katikati), Mwakilishi Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Maifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia) pamoja na Katibu Tawala wilayani Kibondo (kushoto) wakiwa kwenye hafla fupi ya kufuatilia shughuli zinazofanywa na shirika la KIVULINI wilayani Kibondo.
Kikundi cha ngoma za asili kikitumbuiza baada ya Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mama Elizabeth Jacobsen (hayuko pichani). Linaloonekana nyuma ni jengo la polisi kitengo cha dawati la jinsia na watoto wilayani Kibondo lililojengwa kwa ufadhili wa shirika la UN Women kupitia Serikali ya Norway ili kusaidia utatuzi wa migogoro na kesi za ukatili wa kijinsia kwa wasichana na wanawake wilayani humo.
Kikundi cha ngoma za asili kikitumbuiza
Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mama Elizabeth Jacobsen (wa tatu kulia waliokaa) na viongozi mbalimbali alioambatana nao akiwa kwenye picha ya pamoja na wanaharakati wa kujitolea wilayani Kibondo ambao wanajengewa uwezo na shirika la KIVULINI ili kusaidia mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa wasichana na wanawake.
Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mama Elizabeth Jacobsen (wa tatu kulia waliokaa), pia alikagua jengo linaloonekana ambalo limejengwa kwa ufadhili wa shirika la UN Women kupitia Serikali ya Norway ili kusaidia utatuzi wa migogoro na kesi za ukatili wa kijinsia kwa wasichana na wanawake wilayani humo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.