LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Mpango ataka chuo cha IFM kujenga majengo yake Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango ameutaka uongozi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha na kuwa na mkakati wa ujenzi wa majengo yake mkoani Mwanza badala ya kuendelea kutoa elimu katika majengo ya kukodi ili kupunguza gharama za uendeshaji wa chuo.

Waziri Mpango aliyasema hayo Disemba 04, 2020 kwenye mahafali ya saba ya wahitimu wa chuo hicho kampasi ya Mwanza huku akiwataka wahitimu hao wakateseke kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi na hatimaye kulifikisha Taifa katika uchumi wa juu katika kipindi kifupi kijacho.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akizungumza kwenye mahafali hayo.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha IFM, Prof. Emmanuel Mjema aliwahimiza wahitimu wao kuwa mabalozi wazuri wa chuo hicho kwa kufanya kazi kwa bidii.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (wa pili kulia), Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha IFM Prof. Emmanuel Mjema (kulia), Mkuu wa Chuo cha IFM Prof. Tadeo Satta (wa pili kushoto) pamoja na Mkuu wa Wilaya Nyamagana Dkt. Philis Nyingi (kushoto) aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella.
Wahitimu mbalimbali wa chuo cha IFM kampasi ya Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.