LIVE STREAM ADS

Header Ads

Duh! UVCCM waibua shule nyingine, wanafunzi wanakaa chini, wanasomea nje

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Viongozi na wanachama wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, wameshiriki shughuli ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Bulale pamoja na kukagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Bulale katika Kata ya Buhongwa.

Hatua hiyo ni sehemu ya shughuli mbalimbali za kuhamasisha maendeleo katika kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 44 tangu kuasisiwa kwa Chama cha Mapinduzi yanayotarajiwa kufanyika Februari 05, 2021.
Wakiwa katika Shule ya Msingi Bulale, viongozi wa jumuiya hiyo chini ya Katibu wake, Malanyingi Matukuta wameshtushwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliosababisha upungufu wa vyumba vya madarasa.
Mwonekano wa majengo ya zamani katika Shule ya Msingi Bulale jijini Mwanza.
Mwonekano wa majengo mapya katika Shule ya Msingi Bulale jijini Mwanza ambapo Serikali imetoa shilingi milioni 20 ili kugharamia majengo hayo kwa ajili ya kuondoa msongamano wa wanafunzi darasani.
Baadhi ya waalimu wakiendelea na majukumu yao nje ya ofisi kutokana na Shule ya Msingi Bulale kuwa na upungufu wa Ofisi kwa ajili ya waalimu.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.