LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mabinti wa Chuo cha SAUT Mwanza warejesha matumaini kwa mwenzao

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mabinti wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) tawi la Malimbe jijini Mwanza kupitia umoja wao 'Saut Ladies Club' wameanzisha vuguvugu la kuwasaidia mabinti wenzao wenye uhitaji ili nao watiminde ndoto zao kielimu.

Katika uzinduzi rasmi wa klabu hiyo uliofanyika Januari 24, 2021 kwenye viwanja vya Laira Odinga chuoni hapo, mgeni rasmi Flora Magabe ambaye ni Mkurugenzi wa taasisi ya Wanawake na Hatamu aliendesha harambee fupi iliyofanikisha mmoja wa mabinti wenye uhitaji kupata ufadhili gharama za masomo pamoja na hosteli.

Mwenyekiti wa Saut Ladies, Rosemary Wolfgang alisema umoja huo umelenga kuwasaidia mabinti ambao wana changamoto za kiuchumi ili wajikwamue kupitia shughuli mbalimbali za kiujasiriamali na hatimaye kutimiza ndoto zao kielimu.

Katika uzinduzi huo, mabinti wa SAUT Ladies walishiriki zoezi la kuchangia damu, kupima afya bure katika banda la Hospitali ya St. Clare na pia kupata elimu ya huduma za kifedha katika banda la benki ya CRDB.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mgeni rasmi Flora Mabage ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanawake na Hatamu na pia Katibu wa Mbunge Jimbo la Nyamagana akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwakilishi wa Makamu Mkuu wa Chuo cha SAUT akitoa salamu zake kwenye hafla hiyo.
Wadau mbalimbali walichangia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kuwasaidia mabinti wenye uhitaji kupitia zoezi la kukata keki lililoongozwa na mgeni rasmi.
Mgeni rasmi Flora Mabage ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanawake na Hatamu na pia Katibu wa Mbunge Jimbo la Nyamagana akikagua shughuli mbalimbali za mabinti wajasiriamali wa SAUT.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.