LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Nyamagana awataka madiwani kutimiza wajibu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Wilaya Nyamagana mkoani Mwanza, Dkt. Philis Nyimbi amewataka madiwani wa halmashauri ya Jiji la Mwanza kuhakikisha wanatimiza vyema wajibu wao kwa kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Dkt. Nyimbi aliyasema hayo Machi 01, 2021 wakati akizungumza kwenye baraza la madiwani wa halmashauri hiyo na kueleza kushangazwa na baadhi ya hoja ikiwemo ukosefu wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Mabatini B na kuagiza ishughulikiwe haraka.

"Unaposema hakuna choo hapo unatutuma Seriakali Kuu tukafunge hiyo shule maana wanafunzi wanajisaidia wapi" alihoji Dkt. Nyimbi huku akimuagiza Afisa Elimu Msingi kwenda kukagua shule hiyo baada ya kikao hicho na kumpa taarifa mapema.

Awali diwani wa viti maalum, Anifa Mwita alihoji uwepo wa taarifa kwenye makabrasha inayoonyesha shule hiyo haina vyoo na wanafunzi wanatumia vyoo jirani vya shule ya msingi Mabatini A na kuhoji halmashauri ina mkakati gani kujenga vyoo shuleni hapo.

Akijibu swali hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba alisema madiwani ndiyo wenyeviti wa kamati za maendeleo ya Kata hivyo wanapaswa kueleza wamechukua hatua gani kabla ya kwenda kuhoji kwenye baraza na kuwahimiza kwenda kuwahamasisha wananchi kuanzisha miradi ya maendeleo na halmashauri itatimiza wajibu wake wa kuikamilisha.

Naye Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine alisema madiwani wanao wajibu mkubwa katika kuwashirikisha wananchi kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo na hivyo kuondoa mzigo mkubwa wa kutegemea Serikali pekee kutekeleza miradi hiyo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba (kulia) akizungumza kwenye kikao hicho. Kushoto ni Mstahiki Meya wa Halmashauri hiyo, Sima Costantine.
Mstahiki Meya wa Jiji la Meya, Sima Costantine akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo.
Diwani wa Kata ya Isamilo, Charles Nyamasiriri (kulia) akichangia hoja kwenye kikao hicho.
Diwani wa Kata ya Nyamagana, Bhiku Kotecha akizungumza kwenye kikao hicho.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Sima Costantine (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Kiomoni Kibamba (kulia) wakiwa kwenye kikao hicho.
Naibu Meya wa Halmashari ya Jiji la Mwanza, Lordrick Nyoye (kushoto) pamoja na Mstahiki Meya wa Halmashauri hiyo, Sima Costantine wakiwa kwenye kikao hicho.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa Mwanza anayewakilisha kundi la vijana Ng'wasi Kamani (kushoto), madiwani na watendaji mbalimbali wakifuatilia kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Kiomoni Kibamba akizungumza kwenye kikao hicho. 
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.