LIVE STREAM ADS

Header Ads

UVCCM Nyamagana wampata Mwenyekiti mpya

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkutano Mkuu Maalum wa UVCCM Wilaya Nyamagana mkoani Mwanza umemchagua kwa kishindo Boniphace Zephania Boniphace kuwa Mwenyekiti wa jumuiya hiyo akiwapiku Hassan Hussein Mambosasa pamoja na Kisali Sudy Simba.

Uchaguzi huo ulifanyika Jumamosi Machi 13, 2021 baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Philipo Magori kufariki duniani Agosti 2020 hivyo ulilenga kuziba nafasi hiyo hadi utakapofanyika Uchaguzi Mkuu mwakani 2022.

Msimamizi wa Uchaguzi huo, Richard Kashilimu ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCC Taifa alisema kulikuwa na jumla ya wapiga kura 357, kura mbili ziliharibika na kura halali zilikuwa 355.

“Hassan Hussein Mambosasa amepata kura 29, Kisali Sudy Simba amepata kura 79 na Boniphace Zephania Boniphace amepata kura 247 hivyo kwa mamlaka niliyonayo namtangaza kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Nyamagana” Kashilimu alisoma matokeo hayo huku ukumbi mzima ukizizima kwa shangwe.

Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi huo ambaye pia ni Katibu wa UVCCM Wilaya Nyamagana, Malanyingi Matukuta alisema jumla ya wagombea 29 walichukua fomu na waliorejesha walikuwa 25 ambapo walifanyiwa usaili ngazi ya wilaya na kubaki 23 ambao majina yao yalifanyiwa mchujo ngazi ya Mkoa na kubaki majina matatu ambayo ni Boniphace Zephania, Hassan Hussein na Kisali Simba.

Awali akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Nyamagana, Zebedayo Athuman aliwataka vijana wa jumuiya hiyo kujitambua na kutimiza vyema wajibu wao na si kutumika ovyo ikiwemo kubeba ‘brifkesi’ za wakubwa.

Baada ya matokeo hayo wagombea pamoja na mshindi wa nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya Nyamagana walisema uchaguzi umeisha na tofauti za kusaka kura zilizokuwepo pia zimekwisha hivyo kazi iliyo mbele yao ni kushirikiana ili kuijenga jumuiya yao.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti mpya wa UVCCM Wilaya ya Nyamagana, Boniphace Zephania Boniphace akitoa shukurani baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo.
Kutoka kushoto ni Kisali Sudy Simba, Boniphace Zephania Boniphace na Hassan Hussein Mambosasa.
Mkurugenzi wa Uchaguzi huo ambaye pia ni Katibu wa UVCCM Wilaya Nyamagana, Malanyingi Matukuta akizungumza baada ya uchaguzi huo.
Mwenyekiti mpya wa UVCCM Wilaya Nyamagana (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa jumuiya hiyo.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye oicha ya pamoja.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.