Shirika la KIVULINI lawakutanisha wadau kusaka mwarobaini wa mimba kwa wanafunzi
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI limewakutanisha wadau mbalimbali katika Wilaya Ilemela mkoani Mwanza kwa lengo la kupanga mikakati ya pamoja itakayosaidia kutokomeza mimba katika umri mdogo hususani kwa wanafunzi.
Hatua hiyo inakuja wakati takwimu kutoka jeshi la polisi zikionyesha kuwa katika kipindi cha mwaka 2020 kulikuwa na takribani wanafunzi 50 wa kike waliopata mimba wilayani Ilemela huku kwa Mkoa Mwanza kukiwa na zaidi ya wanafunzi wa kike 600 waliopata mimba.
Shirika la KIVULINI linatekeleza mradi wa “Sauti Yangu, Haki Yangu” ukilenga kutokomeza mimba katika umri mdogo katika Kata za Bugogwa, Sangabuye na Kayenze wilayani Ilemela ambapo wadau mbalimbali wakiwemo wazazi, wanafunzi, waalimu, polisi, maafisa ustawi wa jamii, viongozi wa Mitaa na Kata wanashiriki ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akiongoza majadiliano katika kikao hicho.
Afisa Programu kutoka Shirika la KIVULINI, Magreth Kadwela akiwasilisha mada kwenye kikao hicho cha wadau kwa ajili ya kupanga mikakati ya kutokomeza mimba katika umri mdogo wilayani Ilemela.
Wadau wakiwa kwenye kikao hicho.
Wanafunzi ni miongoni mwa wadau walioshiriki kikao hicho.
Mmoja wa wanafunzi akichangia mada kwenye kikao hicho.
Wadau mbalimbali wilayani Ilemela wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: