LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Nyimbi akerwa na uchafu soko la Mirongo, atoa maagizo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Wilaya Nyamagana mkoani Mwanza, Dkt. Philis Nyimbi ameeleza kutoridhishwa na hali ya mrundikano wa uchafu katika soko la Mirongo jijini Mwanza na kuagiza kila mfanyabishara sokoni hapo kuimarisha usafi katika eneo lake.

Nyimbi alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kuongoza zoezi la kufanya usafi sokoni hapo huku akimwagiza Afisa Afya Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Mtendaji Kata ya Mirongo pamoja na viongozi wa soko hilo kuhakikisha wanasimamia zoezi la usafi jumamosi ya kila wiki pamoja na jumamosi ya kila mwisho ya kila mwezi.
Tazama BMG TV hapa cbini

No comments:

Powered by Blogger.