LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kijana auwawa, nyumba ya Mwenyekiti yabomolewa. DC Nyamagana atoa onyo kali

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Kundi la vijana limevamia nyumba ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Ihushi Kata ya Kishiri jijini Mwanza, Kulwa Selemani na kubomoa nyumba yake kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha kijana George Kusekwa (17) mkazi wa Mtaa huo aliyefariki kwa kudaiwa kupigwa kutokana na tuhuma za wizi wa ndala.

Aidha vijana hao wanadaiwa kuzuia mwili wa kijana aliyeuwawa usisarishwe kwenda kuzikwa na kuupeleka nyumbani kwa Mwenyekiti huyo kwa madai kwamba Mwenyekiti huyo na askari mgambo wa Mtaa wake walihusika na kifo hicho.

Kufuatia hali hiyo, Kamati ya Usalama Wilaya Nyamagana ikiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Philisi Nyimbi imefika mtaani hapo na kuonya tabia ya baadhi ya wananchi kujichukulia sheria badala ya kuripoti matukio ya uhalifu kwenye vyombo vya dola.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.