LIVE STREAM ADS

Header Ads

Watuhumiwa wa wizi wa umeme waingia matatani jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Oparesheni ya kushtukiza iliyofanywa na maafisa wa Tanesco kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoani Mwanza imebaini zaidi ya nyumba 20 katika Mtaa wa Misheni Kata ya Pamba jijini Mwanza kuunganishiwa nishati ya umeme kinyemela.

Akizungumza baada ya oparesheni hiyo, Mdhibiti Mapato TANESCO Mkoa Mwanza Mhandisi Rajabu Marwa alisema hatua hiyo inalihujumu shirika na hivyo kulididimiza ambapo alitoa wito kwa wananchi kufuata taratibu ili kuunganishiwa nishati ya umeme.

Mhandisi Marwa alisema watuhumiwa waliokamatwa kwenye oparesheni hiyo watafikishwa mbele ya sheria ili kujibu makosa yanayowakabili na pia kusaidia kuwabaini vishoka wanaoshirikiana nao kulihujumu shirika.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Tazama oicha mbalimbali wakati wa oparesheni hiyo iliyotamatika usiku wa manane...
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.