LIVE STREAM ADS

Header Ads

Jahazi lililotengenezwa kwa taka lawasili Mwanza kupitia Ziwa Victoria

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Jahazi maalumu lililotengenezwa kwa takataka za plastiki pamoja na ndara limekamilisha safari yake ya kuzunguka nchi za Kenya, Uganda na Tanzania kupitia Ziwa Victoria baada ya kuwasili jijini Mwanza lengo likiwa ni kufikisha elimu juu ya madhara yatokanayo na bidhaa za plastiki.

Hafla ya kupokea jahazi hilo iliambatana na uzinduzi wa kampeni ya kupambana na taka za plastiki katika ukanda wa Ziwa Victoria ikiwa ni ushirikiano wa pamoja baina ya wadau mbalimbali ikiwemo shirika la EMEDO pamoja na Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Tazama picha mbalimbali kwenye hafla hiyo...
Mkurugenzi wa shirika la EMEDO, Editrudith Lukanga akitoa salamu kwenye hafla hiyo.
Afisa Mazingira Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Fanuel Kasenene akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kutoa elimu kwa wananchi kutambua madhara ya bidhaa za plastiki.
Mkuu wa Idara ya Usafi na Mzingira Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Danford Kamenya (kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya kutoa elimu kuhusiana na madhara ya matumizi ya bidhaa za plastiki kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (hayuko pichani). Kulia ni Mkurugenzi wa shirika la EMEDO, Editrudith Lukanga.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.