LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia Suluhu Hassan mgeni rasmi Mei Mosi 2021 kitaifa Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Maadhimishi ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yanatarajiwa kufanyika kitaifa katika uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza, Mei Mosi 2021 huku mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Aprili 12, 2021 jijini Mwanza, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Nyamuhokya alisema maadhimisho hayo yatatanguliwa na shughuli mbalimbali ikiwemo makongamano, michezo na maonesho ya usalama mahala pa kazi siku 10 kabla ya kilele.

Nyamuhokya aliongeza kuwa maadhimisho hayo pia yatakuwa maalumu kwa ajili ya wafanyakazi kupitia risala yao kueleza masuala mbalimbali yanayowahusu ikiwemo ongezeko la mishahara mbele ya mgeni rasmi.

Naye Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella aliwahakikishia TUCTA ushirikiano wa kutosha kwenye maandalizi ya maadhimisho hayo akisema Mkoa wa Mwanza utatimiza wajibu wake vyema kwa kushirikiana na mikoa jirani ya Kanda ya Ziwa.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (wa tatu kushoto) wakiwa kwenye kikao hicho cha awali cha maandalizi ya maadhimisho ya Mei Mosi 2021.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.