LIVE STREAM ADS

Header Ads

Katambi aipongeza TANESCO, ataka waajiri kuzingatia usalama kazini

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Afisa Mkuu wa Afya na Usalama Mahala pa Kazi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Makao Makuu, Nelson Mnyanyi (wa pili kulia) akimweleza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Patrobas Katambi (wa kwanza kushoto) jitihada zinazofanywa na shirika hilo katika kuimarisha usalama wa afya kwa wafanyakazi pamoja na jamii.

Ni baada ya Naibu Waziri Katambi kutembelea Maonesho ya Siku ya Usalama wa Afya Mahala pa Kazi yanayofanyika kitaifa katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza kuanzia Aprili 27-28, 2021.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), Khadija Mwenda (wa pili kushoto) akitoa pongezi kwa shirika la TANESCO kwa kuzingatia suala la usalama mahala pa kazi.
Afisa Mkuu wa Afya na Usalama Mahala pa Kazi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Makao Makuu, Nelson Mnyanyi (wa kwanza kushoto) akitoa elimu ya usalama mahapa pa kazi kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la shirika hilo.
Wananchi wakipatia elimu kuhusu matumizi sahihi ya nishati ya umeme pamoja na usalama baada ya kutembelea banda la TANESCO.
Wananchi wakipata elimu na vipeperushi kuhusiana na matumizi sahihi ya nishati ya umeme pamoja na usalama baada ya kutembelea banda la TANESCO kwenye Maonesho ya Siku ya Usalama wa Afya Mahala pa Kazi yaliyoanza Aprili 26-28, 2021 jijini Mwanza.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Patrobas Katambi amezitaka taasisi mbalimbali za umma na binafsi kuhakikisha zinazingatia suala la usalama wa afya na mahala pa kazi kwa wafanyakazi wake ili kuwaepusha na madhara yanayoweza kuwakabili.

Katambi aliyasema hayo Aprili 27, 2021 alipotembelea banda la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwenye Maonesho ya Siku ya Usalama wa Afya Mahala pa Kazi yanayofanyika kitaifa katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Alisema usalama mahala pa kazi ni muhimu kwa wafanyakazi na wananchi kwa jumla hivyo waajiri wanapaswa kuzingatia hilo huku akiipongeza TANESCO kwa kuendelea kutoa elimu ya usalama ili kuwaepusha wafanyakazi na wananchi kutokana na madhara mbalimbali pamoja na jitihada zake za kuendelea kusambaza nishati ya umeme kote nchini.

Naye Afisa Mkuu wa Afya na Usalama Mahala pa Kazi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Makao Makuu, Nelson Mnyanyi alisema shirika hilo limekuwa likitoa elimu ya usalama kwa wananchi ikiwemo kutosegelea ama kuchezea nyaya za umeme.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), Khadija Mwenda alisema bado kuna uelewa mdogo kwa baadhi ya taasisi pamoja na wananchi katika kuchukua tahadhari kuhusiana na usalama mahala pa kazi hivyo elimu zaidi inapaswa kuendelea kutolewa ili kuwaweka salama wafanyakazi pamoja na wananchi.

No comments:

Powered by Blogger.