LIVE STREAM ADS

Header Ads

TBS yawajengea uwezo wajasiriamali Kahama, Shinyanga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na Kadama Malunde – Malunde 1 Blog
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetoa elimu kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga katika mnyororo wa thamani kuhusu kanuni bora za uzalishaji,matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Jumanne Aprili 27, 2021 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama na kukutanisha wajasiriamali 100 wanaojihusisha na bidhaa ya Mchele ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha.

Akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha aliishukuru TBS kwa kukutana na wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele akieleza kuwa ni kundi la wajasiriamali ambao ni sehemu muhimu katika sekta binafsi inayochangia pato la taifa,kuongeza ajira na kuondoa umaskini nchini.

“Wilaya ya Kahama ni moja ya wilaya za kimkakati katika uwekezaji mkubwa katika sekta ya kilimo, madini na biashara, hivyo basi uzalishaji,uuzaji na usambazaji wa mchele ni sehemu ya shughuli kuu kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wakubwa katika wilaya ya Kahama”,alisema Macha.

Licha ya kuwataka washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia ubora,viwango na usalama pia aliwakumbusha kuwa waaminifu kwa wateja wao kwa kuepuka kuchanganya mchele kutoka maeneo tofauti na kuuza kwa bei juu.

Aidha aliwasihi wafanyabiashara wa mchele kuwa wazalendo na kuepuka kushirikiana na wafanyabiashara kutoka nje ya nchi wanaokuja na vifungashio vyao na kutambulisha mchele wa Tanzania kuwa unazalishwa katika nchi hizo akibainisha kuwa kitendo hicho ni kuhujumu uchumi wa nchi.

Kwa upande wake, Meneja wa Utafiti na Mafunzo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.Hamisi Sudi Mwanasala alisema TBS inataka bidhaa nzuri zifungwe kwenye vifungashio sahihi zikiwa na taarifa sahihi ili kulinda afya za watumiaji.

Alisema TBS inaendelea kutoa elimu kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali nchini ili kuhakikisha kuwa wanapata elimu na utaalamu kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio ili kuleta ushindani na kukuza uchumi wa nchi.

Mafunzo hayo yameandaliwa na TBS kama moja ya utekelezaji wa makubaliano ya kikao cha wadau katika mpaka wa Sirari ambacho kiliadhimia TBS kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wasindikaji na wadau wa mchele katika Kanda ya Ziwa.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akifungua Mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama leo Jumanne Aprili 27,2021.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akifungua Mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakifuatilia mafunzo kuhusu kanuni bora za uzalishaji,matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Meneja wa Utafiti na Mafunzo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.Hamisi Sudi Mwanasala akizungumza wakati wa Mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Meneja wa TBS Kanda ya Ziwa Joseph Ismail Mwaipaja akizungumza wakati wa Mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Katibu wa Wamiliki wa Mashine za Kukoboa Mpunga Malunga, Mjini Kahama, Michael Nyahiti akizungumza wakati wa Mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Meneja wa Utafiti na Mafunzo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.Hamisi Sudi Mwanasala, Meneja wa TBS Kanda ya Ziwa Joseph Ismail Mwaipaja na Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mashine za Kukoboa Mpunga Kagongwa wilayani Kahama (kulia) wakiwa ukumbini.
Kushoto ni Afisa Mdhibiti Ubora TBS, Evarist Mrema na Katibu wa Wamiliki wa Mashine za Kukoboa Mpunga Malunga, Mjini Kahama, Michael Nyahiti wakiwa ukumbini.
Afisa Udhibiti Ubora Mkuu TBS, Cunbert Kapilima akiwasilisha mada kuhusu ufungishaji na uhifadhi wa mchele.
Afisa Masoko wa GS1 Tanzania, Shaban Mikongoti akiwasilisha mada kuhusu teknolojia ya usindikaji mchele.
Afisa Afya wa Manispaa ya Kahama, Basil Gervas Kafunja akiwasilisha mada kuhusu kanuni bora za usafi na utunzaji wa mchele.
Afisa Viwango wa TBS, Zena Issa akiwasilisha mada kuhusu utaratibu wa kuthibitisha ubora na faida za kutumia alama za ubora.
Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakifuatilia mafunzo kuhusu kanuni bora za uzalishaji,matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakifuatilia mafunzo kuhusu kanuni bora za uzalishaji,matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Mafunzo yanaendelea.

Maafisa kutoka TBS wakiandika dondoo muhimu kwenye mafunzo ya Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga.
Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakifuatilia mafunzo kuhusu kanuni bora za uzalishaji,matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakifuatilia mafunzo kuhusu kanuni bora za uzalishaji,matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakifuatilia mafunzo kuhusu kanuni bora za uzalishaji,matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.

No comments:

Powered by Blogger.