LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wadau wa Mionzi wapigwa msasa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imeendesha mafunzo ya siku Tano ya kitaifa ya utunzaji na usafirishaji salama wa vyanzo vyenye viasili vya Mionzi (Radioactive source) kwa taasisi mbalimbali zinazojihusisha na usafirishaji wa mionzi nchini.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Dk. Wilbroad Muhogora, Mkuu wa Kanda ya Mashariki alisema mafunzo hayo ni muhimu kwani yatawasaidia washiriki kupata ujuzi wa kuhusu utunzaji na usafirishaji bora na salama wa vyanzo vya mionzi.

Dk Muhogora alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo katika menejimenti ya utunzaji na usafirishaji salama wa vyanzo vya mionzi.

"Usafirishaji wa vyanzo hivi unaweza kusababisha madhara iwapo matakwa ya kiulinzi na usalama hayatazingatiwa wakati wa kuvitunza au kuvisafirisha hivyo mafunzo yatawasaidia kupata uelewa zaidi na kutayarisha mipango ya kinga mionzi wakati wote" alisema Dkt. Muhogora.

Vifaa vyenye mionzi vinatumika nchini katika sekta mbali mbali za kijamii na kiuchumi ikiwemo afya, kilimo, ufugaji, viwanda, barabara ambapo mpaka sasa sasa jumla ya idadi ya vifaa vitoavyo mionzi nchini ni karibu 900 na kati ya hivyo vyanzo vya mionzi vyenye viasili vya mionzi (radioactive sources) ni 400.

Mafunzo hayo yalihudhuriwa na washiriki mbalimbali katika taasisi mbali mbali zinazojihusisha na usafirishaji wa vyanzo vya mionzi nchini.
Na Andrew Chale, Dar

No comments:

Powered by Blogger.