LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mbunge Nyamagana azindua kampeni ya kugawa 'Pedi' kwa wanafunzi wa kike

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Katika kuadhimisha Siku ya Hedhi Salama Duniani, mbunge wa jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (CCM) amezindua awamu ya pili ya kampeni ya ugawaji taulo za kike (pedi) kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari jimboni humo.

Uzinduzi huo umefanyika Mei 28, 2021 katika Shule ya Sekondari Igogo jijini Mwanza ambapo wanafunzi wa kike shuleni hapo wamepatia taulo hizo ikiwa ni jitihada za kuwanusuru na utoro wakati wa hedhi.

“Katika awamu ya kwanza ya ugawaji taulo za kike tuliwafikia zaidi ya wanafunzi elfu kumi ambapo mwaka huu tumelenga kuwafikia wote wa kike katika Shule za kutwa na bweni. Mbunge anataka wanafunzi wa kike wasome bila bughudha wakati wa hedhi” amesema Ahmed Misanga akimwakilisha mbunge Mabula wakati wa uzinduzi huo.

Katibu wa mbunge jimbo la Nyamagana, Flora Mgabe amesema kampeni hiyo imelenga kuwafikia zaidi ya wanafunzi wa kike elfu hamsini ili kuwasaidia wasikose vipindi vya masomo darasani kwani kila mwezi wanakuwa katika hatari ya kutohudhuria shuleni kwa takribani siku nne kwa kukosa taulo za kike.

Naye Afisa Elimu Watu Wazima Mkoa Mwanza, Mwl. Sheja Josephat ametoa rai kwa wazazi na walezi kuwajibika kwa kuhakikisha watoto wao wa kike wanapata taulo za kike badala ya kudhani hedhi ni suala la aibu na watoto hawapaswi kuwashirikisha.

Nao baadhi ya wanafunzi katika Shule hiyo, Vanesa Dickson na Mainda Rajab wamemshukuru mbunge Mabula kwa kuanzisha kampeni hiyo kwani itawasaidia vyema kuhudhuria vipindi huku wenye uwezo duni wakiondokana na adha ya kutumia vitambaa ambavyo si salama kiafya.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Afisa Elimu Watu Wazima Mkoa Mwanza, Mwl. Sheja Josephat akizungumza kwenye uzinduzi huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Albert Chalamila.
Ahmed Misanga akizungumza kwa niaba ya mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula.
Katibu wa mbunge jimbo la Nyamagana, Flora Magabe akieleza umuhimu wa pedi hizo na namna zitakavyowasaidia wanafunzi wa kike hususani wanaoshindwa kumudu gharama za kununua pedi kila mwaka.
Afisa Elimu Watu Wazima Mkoa Mwanza, Mwl. Sheja Josephat akigawa pedi kwa wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari Igogo jijini Mwanza.
Uzinduzi wa kampeni ya kugawa pedi kwa wanafunzi wa kike jijini Mwanza.
Mgeni rasmi Afisa Elimu Watu Wazima Mkoa Mwanza, Mwl. Sheja Josephat (wa tatu kushoto) na viongozi mbalimbali akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari Igogo.
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo.
Katibu wa mbunge jimbo la Nyamagana, Flora Magabe akiwa kwenye picha na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Igogo jijini Mwanza.
Katibu wa mbunge jimbo la Nyamagana, Flora Magabe akiwa kwenye picha na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Igogo.
Katibu wa mbunge jimbo la Nyamagana, Flora Magabe akimkabidhi mche wa mti wa matunda Afisa Elimu Watu Wazima Mkoa Mwanza, Mwl. Sheja Josephat kwa ajili ya kuupanda katika shule ya sekondari Igogo kama ishara ya uzinduzi wa kampeni hiyo.
Mgeni rasmi, Afisa Elimu Watu Wazima Mkoa Mwanza, Mwl. Sheja Josephat akipanda mti kama ishara ya kumbukumbu ya uzinduzi wa kampeni hiyo ya kugawa pedi kwa wanafunzi wa kike jijini Mwanza chini ya ofisi ya mbunge Nyamagana, Stanslaus Mabula.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.