LIVE STREAM ADS

Header Ads

LHRC yawapiga msasa wanahabari kuhusu Sheria za Habari na Haki za Binadamu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mwezeshaji kutoka LHRC, Frida Eligius akizungumza wakati akifungua mafunzo ya Haki za Binadamu na Sheria zinazohusu Tasnia ya Habari kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu na Geita.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Centre - LHRC) kimetoa mafunzo ya Haki za Binadamu na Sheria zinazohusu Tasnia ya Habari (Media Laws) kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu na Geita.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo Jumatatu Julai 12, 2021 Jijini Mwanza, Mwezeshaji kutoka LHRC, Frida Eligius amesema mafunzo hayo ya siku tatu yatawasaidia waandishi hao wa habari kuandika habari kwa weledi zaidi.

"Waandishi wa habari ni kundi muhimu sana katika jamii hivyo ni vyema wakawa na uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya haki za binadamu lakini pia wawe na uelewa kuhusu sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya habari ndiyo maana LHRC tunatoa mafunzo haya ili kulisaidia kundi hili" amesema Eligius.

Nao washiriki wa mafunzo hayo, wameiomba Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu kuziondoa sheria zote ama vipengele vya sheria vinavyolalamikiwa kubinya uhuru wa vyombo vya habari.
Mwezeshaji kutoka LHRC, Frida Eligius akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo.
Mwezeshaji kutoka LHRC, Frida Eligius akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mwezeshaji kutoka LHRC, Frida Eligius akifungua mafunzo hayo.
Mwezeshaji kutoka LHRC, Frida Eligius akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Mwanza.
Washiriki wakimsikiliza Mwezeshaji kutoka LHRC, Frida Eligius.
Waandishi wa habari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu na Geita wakiwa kwenye mafunzo ya Haki za Binadamu na Sheria zinazohusu Tasnia ya Habari.
Waandishi wa habari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Waandishi wa habari wakifuatilia mafunzo hayo.
Waandishi wa habari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wakifuatilia mafunzo hayo.

No comments:

Powered by Blogger.