LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kiongozi wa Mwenge agoma kuzindua mradi wa mamilioni Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Kiongozi wa mbio maalum za Mwenge wa Uhuru 2021, Lt. Josephine Mwambusi amegoma kuzindua mradi wa mizani ya mazao ya samaki katika soko la kimataifa la Mwaloni Kirumba Wilaya Ilemela mkoani Mwanza baada ya kutoridhika na matumizi ya fedha za mradi huo.

Lt. Mwambusi amesema mradi huo uliokamilika mwaka 2019 unagharimu shilingi milioni 373 lakini baada ya ukaguzi, Mwenge wa Uhuru umebaini kasoro mbalimbali kwenye matumizi ya fedha na hivyo kuagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi na kuchukua hatua kwa wahusika.
Na George Binago-GB Pazzo, BMG
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.