LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kiongozi wa Mwenge achukizwa na uchafu Ilemela

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Kiongozi wa mbio maalum za Mwenge wa Uhuru 2021, Lt. Josephine Mwambushi amesononeshwa na uchafu wa mitaro katika barabara mpya ya Mwaloni Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza na kuagiza wahusika kuifanyia usafi kabla ya Mwenge kuizindua.

Lt. Mwambushi alisema uchafu huo ukiendelea kuwepo unaweza kusababisha madhara ya kiafya ikiwemo kipindupindu na malaria pamoja na kuharibu barabara hiyo. 

Ujenzi wa barabara ya Mwaloni ulitekelezwa pamoja na barabara za Sabasaba na Mjimwema ambapo zilizinduliwa kwa pamoja na Mwenge wa Uhuru Julai 04, 2021.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa wakiongozwa na Kiongozi wa Mwenge, Lt. Josehine Mwambushi (kulia) kukagua barabara ya Mwaloni.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.