LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mwanza aagiza Stendi ya Nyegezi kukamilika

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel amekagua ujenzi wa stendi ya mabasi Nyegezi na kuagiza mkandarasi kuongeza kasi ili ikamilike kwa wakati ifikapo mwezi Aprili 2022 na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Aidha ameagiza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) kuanza taratibu za kuboresha miundombinu ya barabara za mitaa zinazozunguka stendi hiyo ili kuondoa adha inayoweza kujitokeza baada ya kukamilika.

Mhandisi Gabriel ameyasema hayo Julai 05, 2021 alipofanya ziara katika stendi hiyo na kuongeza kuwa tayari Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha ili kuhakikisha miradi yote ya kimkakati inakamilika kwa wakati.

Mkandarasi kampuni ya Mohammed Bulders anatekeleza ujenzi wa stendi ya mabasi Nyegenzi kwa gharama ya shilingi bilioni 15.8 fedha kutoka serikalini ambapo kukamilika kwake kutarahisisha huduma kwa wasafiri kutoka ndani na nje ya nchi na kuongeza mapato kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.