LIVE STREAM ADS

Header Ads

Viongozi wa dini himizeni tahadhari dhidi ya Corona- RC Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Eng. Robert Gabriel amewasihi viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa pamoja na kuwahimiza waumini wao kuchukua tahadhari dhidi yamaambukizi ya Corona kwa kuzingatia maelekezo ya kiafya ikiwemo kuvaa barakoa pamoja na kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka.

Eng. Gabriel ametoa ombi hilo Julai 05, 2021 wakati akijitambulisha kwa viongozi wa dini ambapo amekutana Sheikh wa Mkoa Mwanza Hassan Kabeke, Askofu Andrew Gule kutoka kanisa la KKKT Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria pamoja na Askofu Philipo Mafuja wa kanisa la AICT Dayosisi ya Mwanza
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

No comments:

Powered by Blogger.