DC Makilagi apokea Mwenge wa Uhuru wilayani Nyamagana
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Wilaya Nyamagana mkoani Mwanza, Amina Makilagi (kushoto) Julai 06, 2021 amepokea Mwenge wa Uhuru ukitokea wilayani Ukerewe ambapo ukiwa katika Wilaya hiyo utapitia miradi tisa ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 8.1 sawa na kilomita 40.7.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Tazama picha viongozi mbalimbali wakiulaki Mwenge wa Uhuru wilayani Nyamagana.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine ni miongoni mwa viongozi waliojitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru uliowasili katika Wilaya Nyamagana.
Mwenge wa Uhuru ukiwasili wilayani Ilemela ukitokea wilayani Ukerewe.
Wananchi na viongozi mbalimbali wilayani Nyamagana wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Amina Makilagi ( wa pili kushoto) wakikimbiza Mwenge wa Uhurua baada ya kuwasili kutoka wilayani Ukerewe. Wa pili kulia ni Kiongozi wa Mwenge 2021, Lt. Josephine Mwambashi.
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: