LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2021 wilayani Ilemela

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mwenge Maalum wa Uhuru 2021 umewasili katika Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza kwa ajili ya kupitia, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 28.3

Akipokea mwenge huo katika uwanja wa Shule ya Msingi Kayenze, Mkuu wa Wilaya Ilemela, Hassan Masala amesema utakimbizwa takribani kilomita 57 na kupitia miradi saba ya maendeleo wilayani humo ikiwemo afya, elimu, TEHAMA na miundombinu mbalimbali.

Mwenge Maalum wa Uhuru uliwasili mkoani Mwanza Julai 03, 2021 ukitokea mkoani Simiyu katika mapokezi yaliyofanyika wilayani Magu ambapo Kiongozi wa Mwenge huo kitaiga Lt. Josephine Mwambashi amesisitiza upatikanaji wa nyaraka muhimu katika kila mradi utakaopitwa/ kaguliwa.

Kauli mbiu ya Mbio za Maalum za Mwenge wa Uhuru 2021 ni "Tehama ni Msingi wa Taifa Endelevu, Itumie kwa Usahihi na Uwajibikaji".
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenge wa Uhuru baada ya kuwasili katika Wilaya Ilemela mkoani Mwanza.
Mkuu wa Wilaya Ilemela, Hassan Masala (kushoto) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Magu, Salum Kalii (kulia).
Viongozi mbalimbali wilayani Ilemela wakipokea Mwenge wa Uhuru.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.