LIVE STREAM ADS

Header Ads

Maduka ya Dawa zaidi ya 300 yabainika kuwa na kasoro

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wamiliki na Wasimamizi wa Maduka ya Dawa na Vifaa tiba wa Mkoa wa Songwe wakifuatilia kikao kazi kilicho andaliwa na TMDA kwa ajili ya kuwakumbusha taratibu na sheria za Uhifadhi na utoaji dawa pamoja na utunzaji wa Kumbukumbu.
Mfamasia wa Mkoa wa Songwe John Mfutakamba ameyasema akifuatilia kikao kazi cha wamiliki na wasimamizi wa Maduka ya Dawa na Vifaa tiba kwa Mkoa wa Songwe kilicho andaliwa na TMDA kwa ajili ya kuwakumbusha taratibu na sheria za Uhifadhi na utoaji dawa pamoja na utunzaji wa Kumbukumbu.
Wamiliki na Wasimamizi wa Maduka ya Dawa na Vifaa tiba wa Mkoa wa Songwe wakifuatilia kikao kazi kilicho andaliwa na TMDA kwa ajili ya kuwakumbusha taratibu na sheria za Uhifadhi na utoaji dawa pamoja na utunzaji wa Kumbukumbu.

Na Grace Gwamagobe, Songwe
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwa Kushirikiana na Mkoa wa Songwe imebaini maduka ya dawa na vifaa tiba 312 ambayo yalikuwa yakiendeshwa kinyume na taratibu na sheria mara baada ya kufanya Kaguzi nne katika kipindi cha Mwezi Septemba 2020 hadi Aprili 2021.

Mfamasia wa Mkoa wa Songwe, John Mfutakamba aliyasema hayo Juni 30, 2021 wakati wa kikao kazi cha wamiliki na wasimamizi wa Maduka ya Dawa na Vifaa tiba kwa Mkoa wa Songwe ikiwa ni hatua iliyochukuliwa ili kudhibiti uvunjifu wa sheria uliokuwa unajitokeza hapo awali.

Mfutakamba alisema makosa ambayo yamekuwa yakijirudia mara kwa mara ni pamoja na kutozingatia taratibu na sheria za utoaji na uhifadhi dawa na hatua zilizochukuliwa ni baadhi ya maduka kufikishwa mahakamani na kulipa faini ya shilingi milioni sita wa mujibu wa sheria.

Aliongeza kuwa licha ya hatua za kisheria kuchukuliwa Kikao kazi hicho kilicho andaliwa na TMDA kimelenga kuwakumbusha taratibu na sheria wamiliki hao pia Mkoa unapendekeza mafunzo hayo yawe endelevu na yafanyike kwa ushirikiano na Nchi jirani hususani kwa halmashauri zilizoko mpakani.

Kaimu Meneja wa TMDA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Anitha Mshigati alisema lengo la kikao kazi hicho ni kuwakumbusha wamiliki wa dawa na vifaa tiba kanuni za uhifadhi na usambazaji wa dawa kwakuwa wamekuwa wakifanya kaguzi na kuona mapungufu katika maeneo hayo.

Mshigati alisema baadhi ya wamiliki wamekuwa hawana uelewa wa namna ya uhifadhi na utoaji wa dawa na pia katika kutunza kumbukumbu hivyo wameona ni sahihi kuwakumbusha ili wakifanya kaguzi makosa hayo yapungue au kuisha kabisa.

Aliongeza kuwa mara baada ya kikao kazi hicho TMDA itaendelea na kaguzi za mara kwa mara na wanatarajia kukutana na mapungufu kidogo pia dawa na vifaa tiba vilivyopo Mkoa wa Songwe vitaendelea kupimwa ubora wake kwa kutumia maabara iliyoko Tunduma pia dawa zinazoingizwa nchini zitapimwa.

Mmiliki wa Duka la Dawa la Suma, Israel Mwambene alisema changamoto iliyokuwepo awali ilikuwa ni kukaguliwa bila ya kuwa na elimu ya kutosha ila kupitia mafunzo hayo kuna vitu wamevielewa na hata wakikaguliwa tena watakuwa na uelewa wa kutosha.

Naye Mmiliki wa Duka la Dawa la Daima, Israel Mwakilasa alisema kikao hicho kimewawezesha kujua sheria na taratibu ambazo walikuwa hawazifahamu hapo awali.

No comments:

Powered by Blogger.