LIVE STREAM ADS

Header Ads

Hapakaliki Mwanza kukosa maji, tufanye mapinduzi ya haraka- RC Gabriel

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel amesema haikubaliki wananchi kukosa huduma ya maji safi na salama wakati wanazungukwa na Ziwa Victoria hivyo ni wajibu kwa mamlaka za maji kuhakikisha zinashughulikia suala hilo.

Mhandisi Gabriel aliyasema hayo wakati akipokea mabomba kwa ajili ya utandikaji wa mtandao wa maji kupitia mradi wa Malipo kwa Matokeo (PBR) unaotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).

“Mwanza shida siyo maji, tumezungukwa na Ziwa Victoria hivyo wananchi kukosa maji hakukaliki na ofisini hakuingiliki. RUWASA mmesambaza maji asilimia 64 lakini tunatakiwa kufanya mapinduzi ya haraka ili kufikia asilimia 90” alisisitiza Mhandisi Gabriel.

Naye Meneja wa RUWASA, Mhandisi Immaculata Raphael alisema mradi huo wa PBR unalenga kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama karibu na makazi ya wananchi ambapo unatekelezwa katika Halmashauri za Ilemela, Buchosa, Kwimba, Magu, Nyamagana, Sengerema na Ukerewe.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.