LIVE STREAM ADS

Header Ads

WCF yapunguza tozo kwa waajiri wa sekta binafsi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Dickson Billikwija, Dar es Salaam
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umesema waajiri wa sekta binafsi nchini wamepunguziwa kiwango cha mchango wa wafanyakazi cha mapato ya waajiriwa wao kutoka asilimia 1 hadi asilimia 0.6 huku ukibainisha punguzo la kiwango hicho linaanza kutumika kwa michango ya mwezi Julai mwaka huu.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo, Dkt. John Mduma amesema mabadiliko ya punguzo hilo yamekuja baada ya Bunge la Bajeti la mwaka 2021/22 kuweka bayana ya upunguzaji wa tozo ikiwa utekelezaji wa Blueprint na kwamba madiliko hayo yapo kwa mujibu wa Tangazo la Serikali namba 496G la juni 30 mwaka huu lililotolewa dhamana na waziri husika Jenista Mhagama.

Amebainisha kuwa licha ya punguzo la tozo la uchangiaji katika mfuko huo waajiriwa wa sekta binafsi wataendelea mafao ya fidia kama ilivyokuwa awali kwa mujibu wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi na kanuni zake za mwaka 2016.

Amesisitiza kuwa punguzo hilo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi inayoelekeza mfuko kuboresha mazingira ya biashara na ufanyaji kazi wa sekta binafsi jkwa kuiwekea mazingira rafiki.

Ameongeza kuwa punguzo hilo litakuwa na mchango mkubwa kwa sekta hiyo ikiwemo kupunguza gharama za uendeshaji za waajiri, kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji nchini na kuboresha na kuimarisha mahusiano mazuri kati ya waajiri na WCF.

Amekipongeza Chama cha Waajiri nchini (ATE) kwa mchango mkubwa katika uboreshaji wa huduma za waajiri na kushughulikia masuala ya mbalimabli yahayohusu waajiri na waajiriwa likiwemo suala la tozo.

Dkt. Mduma amesema WCF inamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa maamuzi ya kupunguza tozo kwa waajiri wa sekta binafsi na kulipongeza Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) kuwa mstari mbele kuhakikisha waajiri wanafanya kazi wakiwa na uhakika wa kingaz za mwili.

Aidha, amesema mfuko huo una thamani ya Sh Bilioni 437 na kwamba katika kipindi cha miaka mitano umeendelea kukua hivyo ndani ya miaka 30 utabaki kuwa endelevu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Anselimu Peter amesema mfuko huo un idadi ya wanachama 24,952 na kusisitiza tathmini zinaonyesha kuwa utaendelea kuwa imara kama waajiri wataendelea kuzingatia uchangiaji wa michango ya waajiriwa wao.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini Dkt. Abdulsalaam Omar amesema sekta ya umma huchangia asilimia 0.5 kwa waajiri huku sekta binafsi ikichangia 0.6 na kwamba shughuli za sekta ziko za katika hali hatarishi ukilinganisha na umma.

No comments:

Powered by Blogger.