LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mwenge wa Uhuru watua Misungwi, kupitia miradi tisa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mbio maalum za Mwenge wa Uhuru unaendelea na shughuli zake mkoani Mwanza ambapo Julai 08, 2021 umewasili katika Wilaya Misungwi ukitokea wilayani Sengerema ambapo unatarajiwa kukimbizwa kilomita 83.8 na kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya afya, elimu pamoja na TEHAMA.

Akipokea Mwenge huo, Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy amesema utaweka mawe ya msingi kwenye ujenzi wa miradi miwili, kuzindua miradi mitano pamoja na kukagua uendelevu wa miradi miwili ambapo miradi yote ina thamani ya shilingi bilioni 1.5.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenge wa Uhuru baada ya kuwasili wilayani Misungwi ulizindua shughuli za uvuvi zinazofanywa na kikundi cha vijana cha Wazalendo kilichoufaika na fedha za mkopo shilingi Milioni 12 kutoka Halmashauri ya Misungwi.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy (kushoto) akishiriki mbio za maalum za Mwenge wa Uhuru pamoja na wakimbiza Mwenge kitaifa wakiongozwa na Lt. Josephine Mwambashi.
Mwenge wa Uhuru pia umezindua mfumo wa TEHAMA katika Shule ya Sekondari Idetemya. Itakumbukwa kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 ni "TEHAMA ni Msingi wa Taifa Endelevu, Itumike kwa Usahihi na Uwajibikaji" ikilenga kuchochea matumizi sahihi ya tekonolojia kwa maendeleo ya Taifa.
Mkuu wa Wilaya Sengerema, Senyi Ngaga akizungumza mapema kabla ya kukabidhi Mwenge wa Uhuru katika Wilaya Misungwi.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.