LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shirika la EMEDO lakutana na wadau kujadili athari za janga la Corona

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Shirika la Usimamizi wa Mzingira na Maendeleo (EMEDO) lenye makao yake jijini Mwanza limekutana na wadau mbalimbali wakiwemo wazalishaji na wafanyabiashara wa mazao ya uvuvi na kilimo ili kujadili changamoto zilizojitokeza baada ya janga la Corona na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kukabiliana na changamoto hizo.

Mkurugenzi wa shirika la EMEDO, Editrudith Lukanga amesema warsha hiyo ni sehemu ya utafiti unaofanywa na shirika hilo kwa ajili ya kubaini athari hasi na chanya za janga la Corona katika mifumo ya chakula ili kuja mapendekezo yatakayoleta mabadiliko ya sheria na sera zitakazosaidia biashara ya mazao ya uvuvi na kilimo kuendelea hata wakati wa janga hilo.

Akifungua warsha hiyo, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa Mwanza, Isack Ndassa amewahimiza wadau hao kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona hatua itakayosaidia biashara zao kutoathirika kwa kupoteza wateja.

Nao baadhi ya wadau walioshiriki warsha hiyo wameshauri mamlaka za Serikali kuhimiza ulazima wa wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya Corona ikiwemo kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka kabla ya kuingia ama kutoka maeneo yenye misongamano ikiwemo masokoni huku pia wakiomba vifaa kinga kama barakoa kutolewa bure kwa wananchi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa Mwanza, Isack Ndassa  (katikati) akifungua warsha hiyo.
Mkurugenzi wa shirika la EMEDO, Editrudith Lukanga akizungumza wakati wa warsha hiyo.
Wadau mbalimbali wa uvuvi jijini Mwanza walioshiriki warsha hiyo wakitoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na janga la Corona.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.