LIVE STREAM ADS

Header Ads

BAKITA tengenezeni kanzi Data ya wakalimani itakayofikiwa kwa njia ya Mtandao

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa, akizungumza na wataalam wa lugha, wafanyakazi wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Wakalimani na wananchi walioudhuria hafla ya uzinduzi wa vifaa vya ukalimani iliyofanyika katika ofisi za BAKITA Agosti 21 jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa, akizungumza na wataalam wa lugha, wafanyakazi wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA).
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa, kushoto akikata utepe kuzindua vifaa vya ukalimani katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika ofisi za Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Agosti 21 jijiniDar es Salaam kulia kwake ni Naibu wake Mhe. Pauline Gekul kulia na mwisho ni Kaimu Mtendaji wa BAKITA Bi. Consolata Mushi.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa, kushoto pamoja na Naibu wake Mhe. Pauline Gekul kulia (wamekaa) wakimsikiliza mtaalamu wa masuala ya lugha baada ya hafla ya uzinduzi wa vifaa vya ukalimani iliyofanyika katika ofisi za Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Agosti 21 jijiniDar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa, kulia pamoja na Naibu wake Mhe. Pauline Gekul kushoto, wakimsikiliza mtafasiri wa lugha (mkalimani) baada ya kuzindua vifaa vya ukalimani katika hafla iliyofanyika ofisi za Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Agosti 21 jijiniDar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa, akimtuza mzee Ngatuma Said Ngatuma baada ya kugani ushairi mzuri akiisifia lugha ya Kishwahili wakati wa hafla ya uzinduzi wa vifaa vya ukalimani iliyofanyika katika ofisi za Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Agosti 21 jijiniDar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (katikati ) pamoja na Naibu wake Mhe. Pauline Gekul (wamekaa) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), mara baada ya hafla ya uzinduzi wa vifaa vya ukalimani iliyofanyika katika Ofisi za Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Agosti 21 jijiniDar es Salaam.


Na. Projestus Binamungu, GCU- WHUSM

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa ameuagiza uongozi wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), kutengeneza mifumo ya kielektroniki itakayomuwezesha mtu yeyote anayehitaji huduma ya mkalimani wa lugha na hasa lugha ya Kiswahili, kuipata huduma hiyo kwa njia ya mtandao na kwa haraka zaidi.

Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo Augosti 21 wakati akizindua vifaa vya kuwezesha ukalimani, katika hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika ofisi za Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) jijiniDar es Salaam.

Waziri Bashungwa amesema, Serikali kupitia kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu, imetoa kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 187 kugharamia ununuzi wa vifaa hivyo, ikitarajia kuona mabadiliko chanya ya taaluma hiyo kwa manufaa ya wengi wenye uhitaji na kwa ajili ya uendelezaji wa lugha ya Kiswahili kitaifa na kimataifa.

“Ili kuenenda sawa na uwekezaji huu, nawaagiza BAKITA wekezeni nguvu kwenye kubuni mifumo ya kielekroniki itakayomuwezesha mtu kuomba na kupatiwa mkalimani kwa njia ya mtandao, hatuwezi kwenda kizamani zamani lazima twende kidigitali ndiyo maana halisi ya uwekezaji huu.” alisema Waziri Bashungwa.

Aidha Waziri Bashungwa amesema watanzania wote wanawajibika kuiendeleza zaidi lugha ya Kiswahili kwa kuwa Tanzania ndiyo chimbuko la lugha hiyo.Hivyo kama taifa, lina wajibu wa kuhakikisha wanaohitaji kujua kiswahili wanapatiwa rasilimali mbalimbali zitakazo wawezesha kukielewa na kukitumia kwa usanifu na ufasaha zaidi.

Awali akizungumza katika hafla hiyo Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul amesisitiza matumizi na utunzaji mzuri wa vifaa hivyo ili kutimiza azima ya Serikali ya kuendeleza utaalamu wa ukalimani nchini.

Kwa upande wake kaimu katibu mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Bi. Consolata Mushi, amesema vifaa hivyo vilivyonunuliwa vina uwezo wa kuwezesha jumla ya lugha nane kufanyiwa ukalimani kwa wakati mmoja.

Vifaa hivyo vinajumuisha chombo maalumu kwa ajili ya kuchagua lugha na kuzungumza, seva, vipaza sauti, visikizi, spika, kikuza sauti na mashine ya mkalimani, ambavyo vinaweza kutumiwa na watu thelathini kwa wakati mmoja.

No comments:

Powered by Blogger.