LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kamati ya Siasa Mwanza yataka Soko Kuu likamilike kwa wakati

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Mwanza imeagiza mkandarasi kampuni ya Mohamed Builders kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi wa Soko Kuu jijini Mwanza ili kukamilika kwa wakati na kutoa huduma kwa wananchi.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dkt. Antony Diallo aliyasema hayo Agosti 24, 2021 baada ya kutembelea mradi huo kukagua utekelezaji wake ambapo hadi kukamilika mwezi Aprili 2020 utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 20.

Aidha Kamati hiyo ilishauri baadhi ya marekebisho kufanyika mapema katika mradi huo ambao ulianza kutekelezwa mwezi Oktoba 2020 ikiwemo kutenganisha mlango wa kuingilia na kutokea ndani ya soko hilo.

Naye Mkuu wa Mkoa Mwanza, Robert Gabriel ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati hiyo aliagiza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuanza mikakati ya kuandaa maeneo mengine kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo walio katikati ya jiji kwani soko hilo litakapokamilika litakuwa na nafasi 1,600 za wafanyabiashara hao huku waliopo wakiwa ni zaidi ya elfu 20.

Msimamzi wa mradi huo, Eng. Shuhuda Mnyika aliahidi kumsimamia vyema mkandarasi huyo ili kuhakikisha maagizo hayo yanafanyiwa kazi kwa wakati huku akibainisha kuwa mradi huo umefikia asilimia 41 japo ulipaswa kuwa asilimia 60 na kwamba ulichelewa kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwemo uhaba wa saruji, janga la Corona pamoja na kukutana na mkondo wa maji chini ya ardhi hivyo kuchukua muda mrefu kutafuta njia za kuudhibiti.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.