LIVE STREAM ADS

Header Ads

Namba Tatu azindua kampeni za Uchaguzi Mdogo wilayani Bunda

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mara, Samwel Kiboye 'Namba Tatu' amezindua rasmi kampeni za Uchaguzi Mdogo katika Kata ya Nyeruma wilayani Bunda na kutumia fursa hiyo kumuombea kura mgombea wa chama hicho katika nafasi ya udiwani, Fortenatus Maiga.

Kampeni hizo zinatarajiwa kufanyika hadi Oktoba 08, 2021 na kufuatiwa na siku ya kupiga kura Oktoba 09, 2021 ambapo wananchi watapata fursa ya kumchagua Diwani mwingine baada ya aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo kufariki dunia.

Maeneo mengine ambayo Uchaguzi Mdogo utafanyika ni pamoja na Kata ya Kagera Nkanda katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoa wa Kigoma, Kata ya Kileo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga mkoa wa Kilimanjaro, Kata ya Luduga iliyopo Halmshauri ya Wilaya ya Wanging’ombe mkoa wa Njombe, Kata ya Lyowa iliyopo Halmashauri ya Wilala ya Kalambo Mkoa wa Rukwa na Kata ya Vumilia iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Urambo mkoa wa Tabora.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.