LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mwanza awahimiza wakazi wa Ukara kushiriki Sensa ya Majaribio

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel akiwa ameambatana na watendaji mbalimbali amefika katika Kijiji cha Bugalamila Kata ya Bwisya katika Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe na kuwahamasisha wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwenye zoezi la Sensa ya Majaribio linalofanyika katika Kijiji hicho kuanzia Septemba 08- 19, 2021.

RC Gabriel amesema iwapo wananchi watashiriki ipasavyo kwenye zoezi hilo, itasaidia kubaini utendaji kazi wa mifumo ya kidijitali ikiwemo matumizi ya vishikwambi (I-Pad) vinayotumika kwenye zoezi hilo ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye Sensa ya kitaifa mwakani 2022.

Amesema zoezi la Sensa ya watu na makazi ambalo hufanyika kila baada ya miaka 10 ni muhimu kwani husaidia Serikali kupanga vyema vipaumbele na mikakati mbalimbali ya kuwaletea wananchi maendeleo hivyo ni muhimu wakashiriki kwenye zoezi hilo kuanzia Sensa ya Majaribio ambayo kwa Mkoa Mwanza inafanyika katika Kijiji cha Bugalamila. 

Naye Msimamizi Mkuu wa Sensa ya Majaribio Mkoa Mwanza, Morris Oyuke amesema wananchi wamekuwa na mwitikio mzuri wa kushiriki kwenye zoezi hilo huku akiongeza kuwa mfumo wa kidijitali unaotumika umerahisisha ukusanyaji na utumaji wa taarifa kwa wakati ambapo kaya zaidi ya 300 zinatarajiwa kufikiwa katika Sensa ya Majaribio kijijini Bugalamila.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel aliwahimiza wakazi wa Kijiji cha Bugalamila Kata ya Bwisya kisiwani Ukara kushiriki katika zoezi la Sensa ya Majaribio ambalo kwa Mkoa Mwanza linafanyika katika Kijiji hicho. Hatua hiyo itawezesha utambuzi wa mifumo ya kidijitali ikiwemo matumizi ya vishikwambi (I-Pad) vitakayotumika kwenye Sensa ya kitaifa itakayofanyika mwaka 2022.
Mkuu wa Wilaya Ukerewe, Canal Denis Mwila alisema wananchi wa Kijiji cha Bugalamila wameitikia vizuri zoezi la Sensa ya Majaribio inayofanyika katika Kijiji hicho. Sensa ya Majaribio inafanyika katika mikoa 13 nchini ili kutoa fursa ya maandalizi ya Sensa ya kitaifa mwakani 2022.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Bugalamila Kata ya Bwisya katika Kisiwa cha Ukara aliwahimiza wananchi kushiriki vyema kwenye zoezi la Sensa ya Majaribio linalofanyika katika Kijiji hicho hatua itakayofanikisha Sensa ya kitaifa mwakani 2022 kufanyika kwa ufanisi zaidi.
Wakazi wa Kisiwa cha Ukara wakifuatilia mkutano wa uelimishaji Sensa ya Majaribio.
Baadhi ya wakazi wa Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe wakiwa kwenye mkutano wa uelimishaji kuhusu Sensa ya Majaribio inayofanyika kwa Mkoa Mwanza katika Kisiwa hicho kuanzia Septemba 08-19, 2021 ikiwa ni maandalizi ya kueleka Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2022.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel (kulia waliosimama) na Mkuu wa Wilaya Ukerewe Canal Denis Mwila (kushoto aliyesimama) wakishuhudia zoezi la Sensa ya Majaribio inayofanyika kwa Mkoa Mwanza katika Kijiji cha Bugalamila, Ukara wilayani Ukerewe.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel (kulia) akiongea na baadhi ya wakati wa kisiwa cha Ukara alipotembelea Hospitali ya Bwisya ambapo aliwahimiza kushiriki ipasavyo kwenye zoezi la Sensa pamoja na chanjo ya UVIKO 19 ili kujikinga na janga hilo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel akiwa na viongozi mbalimbali katika makaburi ya baadhi ya waliofariki katika ajali ya kivuko cha MV. Nyerere yaliyopo katika kisiwa cha Ukara.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel wakiwa kwenye mnara wa kumbukumbu ya waliofariki katika ajali ya kivuko cha MV. Nyerere uliopo katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe.
Kivuko kipya cha MV. Ukara II "Hapa Kazi Tu" kinachotoa huduma kati ya kisiwa cha Bugorola na Ukara ikiwa ni mbadala wa kivuko cha MV. Nyerere kilichopinduka Septemba 2018.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.