LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Jafo atoa siku 45 wahusika kuteketeza shehena iliyozuiliwa Dar

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo
ametoa siku arobaini na tano kwa wataalamu wa Bandari, TRA, TBS na NEMC kwa pamoja
kushirikiana kwa mujibu wa sheria kuteketeza kontena za mizigo ya mifuko ya plastiki
iliyopo bandari kavu ya Ubungo jijini Dar es salaam.

Ameyasema hayo alipofanya ziara katika bandari kavu ya Ubungo jijini Dar es salaam na
kusema kuwa kuna kontena za mifuko ya plastiki kadhaa zimeingia na mizigo hii
imetelekezwa hapa bandarini na kwa mujibu wa sheria ya Mazingira, mizigo hii inatakiwa
kuteketezwa.

"Juni 2019 Serikali ilipiga marufuku matumizi ya mifuko hii ya plastiki kwahiyo natoa siku
arobaini na tano kwa vyombo vyote kushirikiana kusimamia zoezi la kuteketeza kontena za
mifuko ya plastiki iliyo kinyume na Sheria ya Tanzania na Uharibifu huu utasimamiwa na
watu wa Mazingira NEMC. Lakini jambo lingine ni kwamba tusiruhusu bidhaa ambazo
hazikubaliki ndani ya nchi yetu kuingizwa, lakini pia nipate ripoti ya kimazingira ni kwa jinsi
gani kazi hii imefanyika" alisema Waziri Jafo. 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Sheria NEMC, Benard Kongola
amesema kuwa waliletewa taarifa kuna wadau wanaomba kununua kontena zilizo bandarini
kusafirisha nje ya nchi kwasababu zilikamatwa zikiwa na mifuko ya plastiki ambayo haikidhi
viwango vya kutumia nchini.

Naye Meneja wa TRA Bandari, Fales Mniko amesema makontena yaliingizwa ikiwa
utekelezaji wa sheria ya marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki umeanza.

"Makontena haya yaaliingizwa kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na nchi
nyingine na hatuwezi tukayauza kwasababu Sheria ya Mazingira imezuia, kwa hiyo hizi
kontena zimeingia kwenye listi ya utaratibu wa kuharibiwa" alisema Mniko.

Kwa mujibu wa kanuni ya plastiki ya mwaka 2019 ya mazingira inapiga marufuku
ungizwaji, usafirishwaji nje ya nchi na uhifadhi wa nchini wa plastiki ambazo hazikidhi
viwango. Kwa taarifa za TRA kontena hizi ziliingia mwaka jana mwishoni na zilikuwa
zinaenda nchini Malawi. Sheria inakataa kuzisafirisha nje ya nchi, itaonekana Tanzania ndo
inasafirisha.

No comments:

Powered by Blogger.