LIVE STREAM ADS

Header Ads

Dkt. Biteko afungua Tamasha la "Ulanga Iherepa". Atoa maagizo ya kuipaisha Ulanga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko ameitaka Tume ya Madini kuhakikisha kuwa kuanzia Novemba Mosi 2021 vibali mbalimbali ikiwemo vya uthaminishaji, ufungaji na usafirishaji wa madini vinaanza kutolewa katika eneo la Mahenge Wilaya Ulanga mkoani Morogoro badala ya wafanyabiashara kusafiri kilomita 312 hadi mjini Morogoro kufuata vibali hivyo.

Dkt. Biteko ametoa agizo hilo Ijumaa Oktoba 22, 2021 wakati akifungua Tamasha la Kuhamasisha Fursa za Uwekezaji katika Wilaya ya Ulanga liitwalo "Ulanga Iherepa (Ulanga Amaizing) yaani Ulanga Inapendeza lililoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Aidha Waziri Biteko amewataka wachimbaji na wafanyabiashara wa madini yakiwemo ya Graphite, Spinel na Rubby katika Wilaya ya Ulanga kuhakikisha wanayaongezea thamani ndani ya Wilaya hiyo kabla ya kuyasafirisha huku akibainisha kuwa wizara yake inatarajia kuanzisha Mkoa wa kimadini katika eneo la Mahenge pamoja na kujenga ofisi mpya ya madini katika eneo hilo ili kurahisisha shughuli na biashara ya madini wilayani humo.

Naye Mkuu wa Wilaya Ulanga, Ngollo Malenya amebainisha fursa mbalimbali zilizo katika Wilaya hiyo kuwa ni pamoja na uwekezaji katika sekta ya kilimo, utalii pamoja na madini na hivyo kutumia Tamasha la "Ulanga Iherepa" kuwakaribisha wadau mbalimbali kuwekezaji wilayani Ulanga.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.