LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kamati yaonya wananchi kuchomewa nyumba maeneo ya Hifadhi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Kamati ya pamoja utatuzi wa migogoro ya ardhi ambayo inaundwa na Mawaziri kutoka Wizara nane nchini, imekutana na viongozi mbalimbali mkoani Geita na kueleza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia baadhi ya maeneo ya Hifadhi yaliyokuwa na migogoro ya kimipaka na Vijiji yamegwe kwa ajili ya matumizi ya wananchi.

Kiongozi wa Kamati hiyo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amebainisha kuwa Kamati hiyo ilibaini migogoro ya kimipaka katika Vijiji 975 nchini ambapo kwa Mkoa wa Geita kuna Vijiji 37 ambapo Rais Samia ameridhia maeneo ya Hifadhi kukwata kwa ajili ya wananchi ingawa Waziri Lukuvi ametahadharisha kuwa baada ya zoezi hilo wananchi wanapaswa kuheshimu mipaka ya Hifadhi itakayowekwa.

Katika hatua nyingine Waziri Lukuvu ameonya matumizi ya nguvu katika Vijiji ambavyo wananchi wanapaswa kupisha shughuli za uhifadhi na kuagiza mamlaka zinazohusika kutowabomolea ama kuwachomea nyumba zao bali ziwape muda wa kuhama kwa hiari ili kutoa fursa kwa wananchi hao kunusuru mali zao.

Kikao hicho kimehudhuliwa na viongozi mbalimbali mkoani Geita wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Rosemary Senyamule, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wabunge akiwemo Doto Biteko kutoka jimbo la Bukombe ambaye pia ni Waziri wa Madini.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Geita, Rosemary Senyamule amewataka viongozi mkoani humo kuwaelimisha wananchi ili kuondokana na migogoro ya ardhi katika maeneo ya uhifadhi.
Mbunge wa Bukombe ambaye pia ni Waziri wa Madini, Doto Biteko akiishukuru Kamati ya pamoja utatuzi wa migogoro ya ardhi wakati wa kikao hicho.
Wakuu wa Wilaya mkoani Geota wakifuatilia kikao hicho.
Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa Geita wakiwa kwenye kikao hicho
Viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge wakifuatilia kikao hicho.
Viongozi mbalimbali mkoani Geita wakiwa kwenye kikao hicho
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.