LIVE STREAM ADS

Header Ads

Dkt. Biteko akagua machimbo ya TIN Kagera, achukua maamuzi magumu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko amefanya ziara katika machimbo ya madini ya TIN yaliyopo katika Kijiji cha Nyaruzumbura Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera kufuatilia mwenendo wa biashara ya madini hayo.

Hatua hiyo inakuja kufuatia jitihada zilizochukuliwa na Serikali za kuondoa changamoto mbalimbali zilizokuwepo hapo awali ikiwemo kununuliwa kwa bei ndogo na hivyo kutowanufaisha wachimbaji.

Akiwa katika machimbo hayo, Dkt. Biteko alifurahi kusikia kwamba bei ya madini ya TIN wilayani Kyerwa imepanda kutoka chini ya shilingi elfu tano kwa kilo moja hadi kufikia zaidi ya shilingi elfu 30.

Katika ziara hiyo, pia Dkt. Biteko alikagua kiwanda cha kuchenjua madini ya TIN pamoja na soko kuu la madini hayo wilayani Kyerwa kabla ya kuzungumza na viongozi, wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ambapo pamoja na mambo mengine aliagiza leseni zote za madini mkoani Kagera ambazo hazifanyi kazi zifutwe na wachimbaji wadogo wapatiwe maeneo hayo badala ya kuhodhiwa bila manufaa.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko akizungumza na wachimbaji, wafanyabiashara na viongozi wa wachimbaji madini katika Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera.
Mkuu wa Wilaya Kyerwa, Rashid Mwaimu akizungumza kwenye kikao hicho ambapo alimshukuru Wazii Biteko kwa hatua za haraka alizochukua kunusuru bei ya madini ya TIN kuporomoka.
Mbunge wa Jimbo wa Kyerwa, Innocent Bilakwate alimuomba Waziri Biteko kusaidia upatikanaji wa maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo wa madini ya TIN ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.
Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Kaea, Lucas Mlekwa akitoa taarifa kuhusiana na sekta ya madini mkoani humo.
Mwonekano wa mtambo/ kiwanda cha kuchenjua madini ya TIN (Bati) cha ATM wilayani Kyerwa.
Sehemu ya mwonekano wa kiwanda cha ATM wilayani Kyerwa.
Msafara wa Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko ukiwasili katika machimbo ya TIN yaliyopo Kijiji cha Nyaruzumbura wilayani Kyerwa.
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko (kulia) akimsikiliza mmoja wa wachimaji wa madini ya TIN wilayani Kyerwa.
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Doto Biteko (kulia) akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo wa Kyerwa, Innocent Bilakwate (kutosho).
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Doto Biteko akipata maelezo alipotembelea kiwanda cha madini ya TIN wilayani Kyera.
Wachimbaji wa madini wilayani Kyerwa wakiwa kwenye kikao na Waziri wa Madini, Dkt. Doto Doto Biteko.
Tazama BMG TV hapa chini
SOMA>>> 

No comments:

Powered by Blogger.