LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia amwaga mabilioni Bukombe, kuchochea miradi zaidi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya shilingi bilioni tano kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya elimu, afya na maji katika Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko ameyasema hayo Oktoba 15, 2021 wakati akizungumza na wakazi wa jimbo hilo katika Kata ya Ushirombo.

"Rais Samia Suluhu Hassan anatutendea wema wote huu ili watu wawe na maendeleo, muombeeni mama huyu, anafanya kazi kubwa kwa ajili yetu, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni" ameeleza Dkt. Biteko. 

Katika kuunga mkono jitihada hizo, Dkt. Biteko ametoa shilingi Milioni moja kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa matundu ya vyoo katika Shule ya Msingi Kiziba, mabati 220 pamoja na saruji mifuko 100 ili kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya Ihulike. Wakati ujenzi unaanza alichangia shilingi milioni mbili.

Pia Dkt. Biteko ametoa mifuko 50 ya sarufi pamoja na matofali 2,000 kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za wananchi za ujenzi wa Shule ya Msingi Shikizi ya Shikalibuga.

Katika hatua nyingine Dkt. Biteko amewahimiza wananchi wa jimbo la Bukombe kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa UVIKO 19 kwa kuzingatia ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya hususani kuwa tayari kuchanjwa chanjo ya kupambana na ugonjwa huo kwani imethibitishwa kuwa ni salama.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.