LIVE STREAM ADS

Header Ads

Musoma vijijini wafikishiwa maji ya bomba majumbani

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wananchi wa jimbo la Musoma vijijini mkoani Mara wameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuwafikishia huduma ya maji ya bomba hadi majumbani.

Wakizungumza katika Vijiji vya Bulinga,Bukima na Wanyere, wamesema kwa sasa wanapata maji wakiwa nyumbani kwa wakati wote.

Wamesema kipindi cha nyuma wamekuwa na shida kubwa ya maji na kuyafata umbali mrefu nyakati za usiku.

Mkazi wa Kijiji Cha Bulinga, Mgesi Kuboja amesema ameunganishiwa maji ya bomba nyumbani ambayo ni safi na salama na yanatoka wakati wote.

Amesema maji kwa sasa sio shida tena na kuishukuru serikali pamoja na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini, Profesa Sospeter Muhongo kwa kuwafikishia maji.

Msimamizi wa mradi wa maji wa Bulinga/Bujaga, Daniel Kulwa amesema wananchi zaidi ya 70 tayari wamefikishiwa maji ya bomba nyumbani na vituo 79 vinatoa maji.

"Tunasimamua mradi vizuri na wananchi wanapata maji wakati wote na tunaishukuru serikali kwa hili la kumtua mama ndoo kichwani" amesema Daniel.

Kwa upande wake Masatu Mfungo wa Kijiji Cha Wanyere Kata ya Suguti amesema kabla ya kuunganishiwa maji ya bomba nyumbani walikuwa wakilazimika kuamka usiku kufata maji kisimani na kukwamisha shughuli nyingine za maendeleo.

Meneja wa Ruwasa wilaya ya Musoma muhandisi, Edward Sironga,amesema miradi ya maji inaendelea Kata 21 za jimbo la Musoma vijijini na ipo katika hatua tofauti.

Amesema serikali imetoa fedha zaidi ya bilioni nane ambazo zinatekeleza miradi ya maji lengo likuwa kumtua mama ndoo kichwani.
Na Shomari Binda, Musoma

No comments:

Powered by Blogger.