LIVE STREAM ADS

Header Ads

Profesa Mahalu aongoza Mdahalo mzito ulioandaliwa na DSIK Tanzania

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Katika kuelekea kwenye Maadhimisho ya Siku ya Akiba Duniani, taasisi ya DSIK Tanzania imeandaa mdahalo na kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wanafunzi, waalimu, viongozi wa dini na wawakilishi wa Saccos jijini Mwanza ili kujadili mchango wa jamii katika kuhamasisha elimu ya fedha na utamaduni wa kujiwekea akiba kwa watoto na vijana.

Mdahalo huo umefanyika Alhamisi Oktoba 28, 2021 na kuongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha SAUT, Prof. Costa Ricky Mahalu baada ya kufunguliwa na Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel.

Mhandisi Gabriel alihimiza taasisi ya DSIK Tanzania kufanya utafiti utakaosaidia elimu ya fedha kuwa na manufaa katika jamii baada ya kuonekana kuwa ukosefu wa elimu hiyo umesababisha vikundi vya wajasiriamali kushindwa kurejesha fedha za mikopo ya asilimia 10 zinazotolewa na Halmashauri kupitia mapato ya ndani.

Maadhimisho ya Wiki ya Akiba Duniani yanatarajiwa kufanyika Oktoba 30, 2021 ambapo kwa Tanzania Taasisi ya DSIK Tanzania imeandaa maadhimisho hayo katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.