LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAMBAYA: WANAOMCHUKIA SAMIA WANAHOFIA MAFANIKIO YAKE

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

KAZI INAONGEA
Dar es Salaam.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdul Kambaya, amesema baadhi ya wanasiasa wanaomkosoa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hawafanyi hivyo kwa sababu ya jinsia yake, bali kwa sababu ya mafanikio na uthubutu wake katika kuongoza nchi.

Akihutubia mkutano wa kampeni ya udiwani wa Kata ya Makurumla, Manispaa ya Ubungo, Kambaya amesema kasi ya maendeleo na uwajibikaji wa Dkt. Samia umevunja mitazamo ya zamani kuhusu uwezo wa wanawake katika uongozi.

“Wanaomchukia Dkt. Samia si kwa sababu ni mwanamke, bali kwa sababu anafanya kazi kwa matokeo. Wamezoea kuona wanawake wakinyamaza, lakini huyu mama ni jasiri na mwenye maono,” amesema Kambaya.

Ameongeza kuwa mafanikio yanayoonekana katika sekta za maji, elimu na afya ni uthibitisho wa dhamira ya serikali chini ya Dkt. Samia kuboresha maisha ya Watanzania.

Kwa upande wake, Profesa Kitila Mkumbo, mgombea ubunge wa Ubungo, amemwelezea Dkt. Samia kama “kiongozi mwenye dira na moyo wa kujenga umoja wa kitaifa,” akisisitiza umuhimu wa wananchi kumpa kura ili aendelee kuimarisha uchumi.

Naye mgombea udiwani wa Kata ya Makurumla, Bakari Kimwanga, ameahidi kuendeleza ushirikiano na serikali katika miradi ya maji na ujenzi wa kingo za Mto China, akisema CCM “inafanya siasa za vitendo, si za maneno.”

No comments:

Powered by Blogger.