LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mfuko wa NHIF waipiga tafu Hospitali ya Wilaya Magu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekabidhi msaada wa mashuka 40 katika Hospitali ya Wilaya Magu mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 20 tangu kuanzishwa kwa mfuko huo mwaka 2001.

Hafla ya kukabidhi msaada huo imefanyika Oktoba 02, 2021 ambapo Kaimu Meneja wa Mfuko wa NHIF Mkoa Mwanza, Paul Bulolo mashuka hayo yatasaidia kuondoa adha ya uhaba wa mashuka kwa wagonjwa wanaolazwa katika Hospitali ya Wilaya Magu.

Akipokea msaada wa mashuka hayo na kuyakabidhi kwa uongozi wa Hospitali hiyo, Mkuu wa Wilaya Magu Salum Kalii aliupongeza uongozi wa NHIF kwa namna unavyoshirikiana na jamii katika kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo za kiafya na kutoa rai kwa wadau wengine kuiga mfano huo.
BMG Habari
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Khalii (katikati) akipokea msaada wa mashuka 40 kutoka kwa Kaimu Meneja Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHlF) Mkoa Mwanza, Paul Bulolo (kushoto) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa mfuko huo.
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Khalii (katikati) akipokea msaada wa mashuka 40 kutoka kwa Kaimu Meneja Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHlF) Mkoa Mwanza, Paul Bulolo (kushoto).
Wafanyakazi wa NHIF Mkoa Mwanza pamoja na Hospitali ya Wilaya Magu wakishuhudia makabidhiano ya msaada wa mashuka baina ya Kaimu Meneja wa NHIF Mkoa Mwanza, Paul Bulolo kwenda na Mkuu wa Wilaya Magu, Salum Kalii.
Wafanyakazi wa NHlF wakitandika kitanda katika Hospitali ya Wilaya ya Magu baada ya kukabidhi msaada wa mashuka 40 katika Hospitali hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.