Mfuko wa NHIF wakabidhi Vyeti kwa Wanahabari
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekabidhi vyeti vya shukurani kwa Waandishi wa Habari nchini Tanzania kupitia Klabu zao za Mikoa ikiwa ni hatua ya Mfuko huo kutambua ushirikiano baina yake na Waandishi wa Habari.
Vyeti hivyo vimekabidhiwa Septemba 24, 2021 jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Mkuu NHIF, Charles Lengeju baada ya kufungua mkutano wa Waandishi wa Habari nchini ulioandaliwa na Mfuko huo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2001.
Kwa upande wa Waandishi wa Habari wa Mkoa Mwanza, cheti chao kimepokelewa na Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko (katikati) akisindikizwa na Mwanahabari Abela. Msikula kutoka TSN (kulia).
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala, Charles Lengeju (kushoto) akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam, Irene Mark wakati wa kukabidhi vyeti kwa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania kwa kutambua mchango wa vyombo vya habari kutoa elimu kwa jamii kuhusu Mfuko huo.

Pia mfuko huo umeandaa bonanza la michezo, Jumamosi Septemba 25, 2021 likishirikisha waandishi wa habari, NHIF pamoja na wadau mbalimbali kwa lengo la kuimarisha mahusiano. Bonanza hilo linafanyika katika viwanja vya Kilimani jijini jijini Dodoma.
Central Press Club.
Picha na Richard Mwaikenda, Dodoma
No comments: