LIVE STREAM ADS

Header Ads

Maadhimisho ya Wiki ya Posta yaanza jijini Dodoma

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Kuwe Bakari akifafanua jambo mbele ya Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Andrew Mathew wakati alipotembelea banda la TCRA katika viwanja vya Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Dodoma katika uzinduzi wa Wiki ya Posta, Oktoba 06, 2021.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Kuwe Bakari akiwasilisha salamu za TCRA wakati wa tukio la uzinduzi wa Duka la Posta Mtandaoni lililofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma. Duka hilo la Mtandaoni limezinduliwa na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na TEHAMA Mhandisi Kundo Mathew katika Wiki ya Posta.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Kuwe Bakari akifafanua jambo mbele ya Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Andrew Mathew, alipotembelea banda la TCRA katika viwanja vya Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma. Wiki ya Posta imezinduliwa jijini Dodoma kuelekea kilele cha Siku ya Posta Oktoba 9, 2021.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Andrew Mathew (Mb), akizindua Duka la Posta Mtandaoni ikiwa siku ya kwanza ya Wiki ya Posta inayoadhimishwa kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Dodoma. 
Picha na TCRA

No comments:

Powered by Blogger.