LIVE STREAM ADS

Header Ads

Majengo aliyosomea Mama Nyerere yahitaji ukarabati

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Majengo ya kilichokuwa Chuo cha Ualimu Sumve Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, alikosoma mjane wa Baba wa Taifa mama Maria Nyerere na baadaye kubadilishwa matumizi kuwa shule ya Sekondari ya Wasichana Sumve yanahitaji kiasi cha shilingi milioni 26 kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati kutokana na kuchakaa baada ya kutofanyiwa ukarabati kwa zaidi ya miaka 30.

Mkuu wa shule hiyo, Clotirida Komenkesha ametoa ombi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ummy Mwalimu kuikarabati shule hiyo kama Serikali ilivyozikarabati baadhi ya shule kongwe nchini zikiwemo Nganza, Bwiru Wasichana na Nsumba mkoani Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.