LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali yamwaga mbegu kwa wakulima

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa kilimo Profesa Adolf Mkenda (wa pili kushoto), akipata maelezo juu ya kilimo na mafuta ya alizeti aina ya Katam, kutoka kwa mkulima Dk. Henry Mmbado (wa pili kulia) mjini Singida, wakati waziri huyo alipotembelea mabanda ya maonesho ya zao la alizeti, kabla ya kugawa mbegu za zao hilo kwa wakulima wa mkoa wa Singida.
Waziri wa kilimo Profesa Adolf Mkenda (kushoto), akiwa ameshikilia mkonge, huku akistaajabu kuona unalimwa na kustawi vema mkoani Singida (kulia) ni wakulima akiwemo Raadhan Kinuasi, baada ya kutoa maeneleo ya kina juu ya zao hilo linalostawi kwa wingi katika halmashauri ya wilaya ya Singida.
Waziri wa kilimo Profesa Adolf Mkenda (wa pili kulia), akipata maelezo juu ya ubora wa mafuta ya alizeti, maelezo yanayotolewa na mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge (wa kwanza kulia), alipotembelea mabanda ya maonesho ya alizeti, kabla ya kugawa mbegu za zao hilo kwa wakulima wa mkoa wa Singida.
Waziri wa kilimo Profesa Adolf Mkenda (wa pili kulia), akipata maelezo juu ya ubora wa mafuta ya alizeti, maelezo yanayotolewa na mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge (wa kwanza kulia), alipotembelea mabanda ya maonesho ya alizeti, kabla ya kugawa mbegu za zao hilo kwa wakulima wa mkoa wa Singida.
Waziri wa kilimo Profesa Adolf Mkenda (kushoto), akiwa ameshikilia mkonge, huku akistaajabu kuona unalimwa na kustawi vema mkoani Singida (kulia) ni wakulima akiwemo Raadhan Kinuasi, baada ya kutoa maeneleo ya kina juu ya zao hilo linalostawi kwa wingi katika halmashauri ya wilaya ya Singida.


Na Elisante John, Singida
Serikali kupitia mradi unaofadhiliwa na mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo (IFAD) katika sekta ya kilimo, imeupatia mkoa wa Singida tani 52 za mbegu ya alizeti, ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa mafuta ya kula nchini, ambalo hulikabili taifa kila mwaka.

Akizungumza kwenye makabidhiano ya mbegu hizo mjini Singida, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu nchini (ASA), Dk. Sophia Kashenge amesema ili kwenda sawa na msimu wa mvua, wizara ya kilimo inafanya mazungumzo na wizara ya ulinzi, kuhakikisha magari ya jeshi la Wananchi (JWTZ), yanatumika kusambaza mbegu hizo ili ziwafikie wakulima kwa wakati.

Dk. Kashenge amefafanua kuwa katika uzinduzi wa ugawaji wa tani 52 za mbegu hizo, ni kwa ajili ya wilaya ya Mkalama na Iramba,ambazo zimewakilisha mikoa mitatu ya kimkakati kwa kilimo cha alizeti, yaani Singida, Simiyu na Dodoma.

Naye mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge, akatumia fursa hiyo kuomba mbegu zaidi, zitakazoweza kutosheleza mahitaji ya mkoa huo, ambazo ni tani 465.2, lakini mpaka sasa tayari serikali ya mkoa imefanikiwa kupokea tani 279.9.

“Mheshimiwa waziri nakuamini sana katika kutekeleza majukumu yako, mpaka sasa umefanya kazi kubwa sana, lakini ombi letu lilikuwa ni tani 465.2 za mbegu, kama umefanikiwa kutuletea tani 279.9…naamini kwa kiasi kilichobaki hakiwezi kukushinda,”alisema Dk. Mahenge.

Kwa upande wake mwakilishi wa mfuko wa maendeleo ya kilimo nchini (IFAD) Jaquleen Machagu, alisema kuwa mbegu hizo ni katika kuwasaidia wakulima walioathiriwa na tatizo la UVICO-19.

Machagu alisema kuwa tangu janga la UVICO-19 liikumbe Dunia, limeathiri sughuli nyingi za uzalishaji mali, ikiwemo Tanzania, huku wakulima wakiwa ni sehemu ya wanhanga wa tatizo hilo.

Kutokana na hali hiyo, mwakilishi huyo wa IFAD hapa nchini amesema kuwa, mfuko huo utaendelea kusaidia wakulima na sekta nzima ya kilimo, kwa lengo la kuboresha na kuinua kazi zinazotekelezwa na mkulima hapa nchini.

Waziri wa kilimo Profesa Adolf Mkenda, amesema pamoja na juhudi zinazofanywa na serikali kuwezesha mbegu ziwafikie wakulima kwa wakati, kitengo cha wakala wa mbegu nchini (ASA) kimeendelea kufanya vema katika kufanikisha zoezi hilo.

Profesa Mkenda amempongeza wakala wa mbegu nchini (ASA) kwa kufanya kazi hiyo kwa ajili ya maslahi ya taifa, kwa lengo la kuongeza mapambano katika kukabilina na tatizo la uhaba wa mafuta ya kula nchini kila mwaka.

Baadhi ya wakulima walionufaika na mbegu hizo, akiwemo Zainabu Nkungu na Ramadhan Kinuasi, wameishukuru serikali na kuahidi kilimo chenye tija katika kuhakikisha wanaongeza uzalishaji wa mbegu za alizeti ili kupunguza ukubwa wa tatizo la mafuta ya kula nchini.

Kwa mujibu wa waziri wa kilimo Profesa Adolf Mkenda, Tanzania hutumia zaidi ya shilingi Bilioni 450/- kila mwaka kugharamia mafuta ya kula kutoka nje ya nchi, ambazo zikiokolewa, zitatumika kutekeleza miradi mingine mbalimbali ya maendeleo.

No comments:

Powered by Blogger.