LIVE STREAM ADS

Header Ads

Majonzi mazito, 14 wapotesha maisha, wakiwemo wanahabari

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Watu 14 wakiwemo waandishi wa habari wa Mkoa Mwanza wamefariki dunia baada ya magari waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso katika eneo la Kalemela Wilaya ya Busega mkoani Simiyu chanzo kikielezwa kuwa ni mwendo kasi.

Ajali hiyo imetokea Januari 11, 2021 majira ya asubuhi kwa kuhusisha gari walilokuwa waandishi wa habari aina ya Land Cruiser lenye nambari za usajili STK 8140 lililokuwa linaelekea wilayani Ukerewe kupitia Bunda kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa Mwanza na lingine ni la abiria aina ya Toyota Hiace lenye nambari T. 283 DER lililokuwa linatokea Lamadi kuelekea mkoani Mwanza.

Miongoni mwa waliofariki ni pamoja na waandishi wa habari ambao ni Husna Milanzi (ITV), Johari Shani (Uhuru Digital), Antony Chuwa (Daily News Digital), Abel Ngapenda (Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza) na Steven Msengi (Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe huku waliojeruhiwa wakiwa ni Tunu Heman (Freelancer) na Vany Charles (Icon TV Online).

Miili ya watu waliofariki imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa Mwanza Sekou Toure huku majeruhi wanne wakiwemo waandishi wa habari wawili wakiendelea na matibabu katika Kituo cha Afya Nassa pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.