LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waandishi wa Habari Mwanza wapata ajali

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Taarifa za awali
Gari la waandishi wetu wa Mkoa wa Mwanza lililokuwa kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza limepata ajali eneo la Busega kwa kugongana na Hiace likiwa linaelekea Ukerewe kwa kupitia Bunda.

Nimeongea na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ndugu Robert Gabriel na amethibitisha kupokea taarifa za watu watano waliokuwa kwenye gari hilo lililobeba waandishi kufariki.

Majina ya wenzetu hao tutayatoa kadri tutakavyofuatilia.

Kwa sasa Mkuu wa Mkoa naye anaelekea eneo la tukio nasi pia tunajipanga kwenda eneo la tukio.
Naomba tuwe watulivu kwa wakati huu, wakati team yetu na ya Mkuu wa Mkoa tunafuatilia tukio hilo.

Edwin Soko
Mwenyekiti
Mwanza Press Club
11.01.2022

Watu 14 wakiwamo waandishi wa habari saba wamefariki dunia baada ya gari la waandishi wa habari iliyokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (RC), Robert Gabriel kugongana na gari ya abiria aina ya Toyota Hiace  katika eneo la Nyamikoma wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu akiwa eneo la tukio, Mkuu wa Wilaya ya Busega (DC), Gabriel Zakaria amethibitisha kutokea vifo hivyo.

Amesema kati ya vifo hivyo kuna vifo vya waandishi wa habari wanne na dereva wa waandishi na watu wengine sita walifariki papo hapo

“Ni kweli ajali hiyo imetokea, watu 11 wamefariki kwenye eneo la tukio wakiwemo waandishi wa habari wanne na dereva na wengine sita waliokuwa kwenye gari lingine” amesema Zakaria na kuongeza

“Dakika chache majeruhi waliopelekwa kwenye kituo cha afya cha Nasa watatu walifariki, wakiwemo wale waandishi wa habari waliokuwa kwenye msafara”  amesema

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyo, Blasius Chatanda amesema yupo katika hospitali ambako majeruhi walikopelekwa akiahidi kuwa atatoa taarifa baadaye.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel naye amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema yuko njiani kuelekea eneo la tukio. #Mwananchi


No comments:

Powered by Blogger.