LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Gwajima kuzindua Kituo cha Watoto Mirongo Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima Februari 09, 2022 anazindua Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto Mirongo kilichopo katika soko la wajasiriamali Mirongo jijini Mwanza.

Ujenzi wa Kituo hicho ulienda sambamba na uboreshaji wa miundombinu ya Soko la Mirongo ambayo ni pamoja na vyoo, mitaro na paa katika eneo la kuuzia bidhaa na hivyo kuondoa adha kwa wajasiriamali katika soko hilo la mbogamboga na matunda ambalo asilimia kubwa wauzaji ni wanawake.

Maboresho hayo yalifanywa na shirika la kutetea haki za wanawake na watoto KIVULINI kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo I4IF, UKAid, IrishAid pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa gharama ya shilingi Milioni 88.

Miundombinu bora katika soko la Mirongo itasaidia wajasiriamali kufanya biashara zao katika mazingira salama na kukuza biashara zao huku Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto kikisaidia kuimarisha usalama wa watoto pindi wazazi wao wanapokuwa kwenye biashara huku pia akina mama wanaonyonyesha wakiwa na eneo maalum la kunyonyeshea.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Akina mama wakifuarahia wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Kituo cha Malezi na Makuzi ya Watoto Mirongo jijini Mwanza.
Akina mama wajasiriamali wakifurahia uzinduzi wa Kituo hicho.
Tazama BMG TV hapa chini

1 comment:

  1. How to Play Casino: Easy Guide to playing slots on
    Casino games are played septcasino.com by 4 players, https://tricktactoe.com/ the average time they take turns is around 14:20. The house is kadangpintar divided into aprcasino three distinct categories: the house

    ReplyDelete

Powered by Blogger.